Juhudi za UM za kulinda amani Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo

30 Machi 2009

Leo hii, tunazungumzia kazi za afisi inayosimamia juhudi kubwa kabisa za kulinda amani za UM huko Africa na kugharimu karibu dola bilioni moja, MONUC.

Watoto - DRCAfisi hiyo ilianzishwa 1999, kusaidia kutekeleza makubaliano ya amani ya Lusaka, kwa kusimamia usitishaji mapigano, kuwapokonya silaha wapiganaji na kuwarudisha katika maisha ya kawaida na kusaidia kutayarisha uchaguzi. Miaka 10 baada kwa msaada wa wafanyakazi elfu 22 wakijeshi na kiraia wa UM, amani imeweza kurudi katika sehemu kubwa ya nchi hiyo, uchaguzi umefanyika na hivi sasa juhudi zinafanyika kuwapokonya silaha wapiganaji na kuwarudisha katika maisha ya kawaida. Abdushakur Aboud amezungumza na mfanyakazi mmoja wa MONUC huko Kindu Ahmed Sharif na kumuliza kwanza hali ya maisha kwa ujumla huko JKK.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter