Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

AU-UM wasafirisha vifaa vya mtihani kwa wanafunzi Darfur

AU-UM wasafirisha vifaa vya mtihani kwa wanafunzi Darfur

Afisi ya pamoja ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika AU na UM huko Darfur UNAMID imesaidia hii leo kusafirisha kwa ndege vifaa vya mtihani kwa shule za secondary za maeneo ya mbali katika jimbo hilo la magharibi ya Sudan linalokumbwa na ghasia.

Hii ni operesheni ya pili kwa UNAMID kufanya kwa ajili ya mtihani wa kukamilisha shule ya sekondari unaofanyika kote Sudan na unatazamiwa kuanza hapo Machi 30. Na kwengineko huko Darfur kundi la watu walokua na silaha wametia moto kambi ya kiyenyeji na kusababisha vifo vya watu wawili na kuharibu mamia ya hifadhi za watu hii leo huko El Geneina na kusababisha hasara kubwa.