Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua za kuimarisha chakula Benin zapongezwa na mtaalamu wa UM

Hatua za kuimarisha chakula Benin zapongezwa na mtaalamu wa UM

Mtaalamu wa UM juu ya haki ya kupata chakula, Olivier De Schutter amepongeza juhudi za Benin kuimarisha usalama wa chakula huku akisisitiza kwamba juhudi hizo zinabidi pia kuimarisha hali ya maisha ya wakazi maskini.

Akizungumza na waandishi habari baada ya ziara yake ya hivi karibuni huko Benin, Bw De Schutter alipongeza juhudi kubwa za serekali za kufufua sekta ya kilimo pamoja na mageuzi ya mashamba. Alisisitiza haja ya kuongeza uzalishaji ili kupunguza nchi kutegemea chakula kutoka njee na hasa kuchukua hatua hiyo wakati huu wa kuongezeka bei za chakula duniani.