KM atoa mwito wa kuachiwa wafanyakazi wa UM

25 Machi 2009

KM Ban Ki-moon, akiungana pamoja na wafanyakazi wengine wa UM wametoa mwito hii leo kuachiliwa huru wafanyakazi 19 wa UM wanaoshikiliwa au hawajulikani walipo kote duniani.

Akizungumza kwenye sherehe za kuadhimisha siku ya kimataifa ya kuwaunga mkono wafungwa na watumishi wasojulikana walipo wa UM alisema, wafanyakazi wa huduma za dharura wanaoajiriwa katika nchi zao na wafanyakazi wa UM ni mionogni mwa wanaolengwa zaidi na kukabiliwa na matukiyo makubwa ya usalama. Bw Ban alitoa mwito kwa mataifa wanachama na makundi kuwachilia huru mara moja watu hao. Kati ya 2007 hadi 2008 kulikua na watu 160 walokamatwa na mamlaka ya usalama wa kitaifa na watu 39 waloshikiliwa na makundi yasiyo ya kiserekali, alieleza Bw Ban.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter