Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, Dominique Strauss-Khan ametoa mwito wa ushirikiano mkubwa zaidi kati ya IMF na Shirika la Kimataifa la Kazi ILO, akisema ushirikiano kati ya taasisi za kimataifa ni muhimu katika kukabiliana na mzozo wa uchumi.

Akihutubia mkutano wa maafisa wakuu wa bodi ya utawala ya ILO, Bw Strauss-Khan kuwepo na ushirikiano na ILO yaani wafanyakazi na wajiri ni muhimu kwa shirika lake, kufuatana na misingi ya kazi za IMF. Alihimiza serekali na taasisi za kimataifa kufanyakazi kwa karibu zaidi kukabiliana na athari za moja kwa moja kutokana na kudumu kwa uchumi.

Shirika la Afya Duniani, WHO limeripoti hii leo kwamba kuna dalili za kupunguka kwa kesi za watu waloambukizwa na kufariki kutokana na ugonjwa wa kipindupindu huko Zimbababwe mnamo miezi miwili iliyopita, lakini alihimiza watu kua macho, kutokana na uwezekano wa ugonjwa kuzuka tena katika baadhi ya maeneo. Kufuatana na takwimu mpya zilizotolewa Ijumatatu, WHO imeeleza kwamba kulikua na kesi elfu 2074 zilizoripotiwa kufikia mwisho wa wiki wa tarehe 14 Marchi, ingawa kiwango kikubwa lakini ni chini kulingana na kesi elfu 3812 wiki iliyotangulia, na kesi elfu 8 kwa wiki mwanzoni mwa Febuari.

Wizara ya Afya na Wakazi ya Misri imetangaza ikithibitisha kwamba mwanamke mwenye umri wa miaka 38 katika wilaya ya Elfath, ameambukizwa na homa ya ndege. Ikithibisha habari hizo imeeleza kwamba mwanamke huo amekua na dalili za homa hiyo alipopatwa na homa na kuumwa na kichwa tangu Marchi 14, na amelazwa hospitali na anapatiwa matibabu. Uchunguzi wa kujua jinsi alivyoambukizwa umethibitisha kwamba alikua karibu na kuku wagonjwa na walofariki kabla ya kua mgonjwa.