Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban anapongeza kuachiliwa mfanyakazi moja wa UM huko Niger

Ban anapongeza kuachiliwa mfanyakazi moja wa UM huko Niger

KM Ban Ki-moon amepongeza hii leo kauchiliwa huru mfanaykazi mmoja wa UM aliyetekwa nyara Niger mwishoni mwa mwaka jana na akarudia tena mwito wake wa kuachiliwa huru wafanyakazi wengine wawili pamoja na mwakilishi wa UM nchini humo, Robert Fowler kutoka Canada.

Msemaji wa KM amesema Bw Ban amefurahi kuachiliwa kwa Soumana Mounkaila dereva wa moja wapo wawafanyakazi aliyetekwa nyara huko Niger tarehe 14 disemba. Katika Taarifa hiyo KM amepongeza juhudi za serekali na watu walosaidia kuachiliwa kwa mfanyakazi huyo aliyetekwa nyara karibu na mji mkuu wa Niamey.