Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aondoka kwa ziara ya mataifa sita ya Ulaya na Mashariki ya Kati

Ban aondoka kwa ziara ya mataifa sita ya Ulaya na Mashariki ya Kati

KM Ban Ki-moon ataanza ziara ya mataifa sita ya Ulaya na Mashariki ya Kati akianza huko Rashia ambako mjini Moscow atahudhuria mkutano juu ya Afghanistan.

Mkutano huo utazingatia juu ya athari za hali ya vita nchini humo kwa mataifa jirani, pamoja na kutathmini nia za pamoja kukabiliana na vitisho kama vile ugaidi biashara haramu ya madawa ya kulevya na uhalifu wa magengi. KM anatarajiwa pia kuelekea Doha, Qatar kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Umoja wa nchi za Kiarabu kujadili utaratibu wa amani wa Mashariki ya Kati, Lebanon, Irak, Sudan na Somalia. Kutokea Qatar, Bw Ban atahudhuria mkutano wa kimataifa juu ya Afghanistan huko The Hague kabla ya kushiriki katika mkutano wa kundi la G20 huko London. KM atatembelea pia Ufaransa na Uturuki.