Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID inaeleza kuongezeka kwa uhalifu huko Darfur

UNAMID inaeleza kuongezeka kwa uhalifu huko Darfur

Afisi ya pamoja ya UM na Au ya kulinda amani huko Darfur UNAMID, imeripoti hii leo kuongezeka kwa vitendo vya wizi wa utumiaji nguvu, uhalifu, uvamizi dhidi ya wafanyakazi wa UM na raia katika maeneo yote ya jimbo la Darfur huko Sudan.

UNAMID peacekeeperSiku ya jumatano wafanyakzi wawili wakiwa ndani ya gari la UM walishambuliwa na watu walokua na mavazi ya kijeshi na kupigwa na kuachwam njiani katika mji wa Nyala mji mkuu wa Darfur ya Kusini.