UM unatafuta dola milioni 244 kuimarisha msaada wa chakula Kenya
Idara ya Chakula Duniani WFP, imetoa mwito Jumatano wa kuchangisha dola milioni 244 ilikuimarisha kazi zake huko Kenya, ambako bei za juu za chakula na ukame zimesababisha watu milioni 3 na nusu kuhitaji mdsaada.
Serekali ilitangaza maafa ya kitaifa mwezi Januari, kufuatia kukosekana mvua katika baadhi ya maeneo ya nchi. Katika taarifa yake WFP inaeleza kwamba familia nyingi zinahangaika kutafuta chakula, hata kupata chakula mara moja kwa siku na wanahitaji msaada wa chakula hadi msimu wa mvua mwaka 2010. WFP inaeleza kwamba watu milioni 3.5 watakaofaidika na msaada huo wanapatikana maeneo ya mashambani.