Matumaini ya mafanikio kwenye mkutano wa ubaguzi mwezi ujao

18 Machi 2009

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa UM, BI Navi Pillay, ameeleza matumaini yake Ijumatano ya kuwepo na maridhiano miongoni mwa mataifa wanachama kwenye mkutano wa mwezi ujao wa kupambana na ubaguzi, kutokana na kutolewa mswada mpya mfupi wa rasimu ya hati ya mwisho ya mkutano.

Mkutano huo utafanyika kuanzia tarehe 22 hadi 24 April huko Geneva utatathmini maendeleo yaliyopatikana tangu mkutano wa kihistoria wa kimataifa wa 2001 dhidi ya ubaguzi, ubaguzi wa rangi, ubaguzi dhidi ya wageni, na masuala yanayohusiana na ubaguzi huko Durban. Wakati wa mkutano na waandishi habari Bi Pillay alisema, ana matumaini kwamba kutokana na kuwasilishwa kwa mswada mfupi zaidi ni mabadiliko makubwa katika kutayarisha mkutano huo. Na anatumaini mataifa yataweza kuridhiana ili kuwepo na mkutano wenye mafanikio ambao utaleta msaada kwa mamilioni ya watu na mamia ya makundi yanayokabiliwa na ubaguzi na aina nyinginezo za unyanyasaji kote duniani.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter