Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAIDS yahimiza mipango ya mchanganyiko kupambana na UKIMWI

UNAIDS yahimiza mipango ya mchanganyiko kupambana na UKIMWI

Kukiwepo na zaidi ya watu 7 400 kila siku wanao ambukizwa na virusi vya HIV, shirika la kupambana na UKIMWI la UM UNAIDS, linasema ni lazima kuwepo na mkakati wa kIchanganyiko ikiwa ni pamoja na utumiaji mipra ya kondom kama chombo muhimu kuzuia kuenea kwa janga la UKIMWI.

Katika taarifa yake iJumatano, idara hiyo imeeleza kwamba ni muhimu kuhamasisha utumiaji kondoms pamoja na kutoa habari na matibabu ya HIV, kutoanza mapenzi mapema, kupunguza kuwa na wapenzi wengi, kuimarisha haki za binadamu na kupunguza unyanyapa kama njia ya kupambana na janga hilo.