17 Machi 2009
Msaada wa dola milioni 16 kutoka kwa serekali ya Japan, utaweza kulisaidia shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, kukabiliana na baadhi ya athari kutokana na mzozo mkubwa wa chakula unaowakabili wahamiaji huko Pembe ya Afrika pamoja na Mashariki na Kusini ya bara hilo.