Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikao cha 53 cha CSW

Kikao cha 53 cha CSW

Leo hii, tunaendelea na mazungumzo juu ya kikao cha 53 cha kamisheni juu ya hali ya Wanawake, kilichomalizika Ijuma tarehe 13, katika makao makuu ya UM.

 Wajumbe kwenye mkutano huo walijadili kwa mapana marefu namna ya kuhamasisha haja ya wanawake na wanaume kufanya kazi pamoja katika majukumu ya malezi, kuwahudumia waathiriwa wa HIV na Ukimwi, pamoja na majukumu ya nyumbani. Wajumbe pia walikiri ile hali ya kuwahusisha zaidi wanaume katika mikutano kama hii, ili wafahamu zaidi matatizo yanayowakabili wanawake hasa katika wakati huu wa mzozo wa kifedha na mabadiliko ya hali ya hewa. Abdushakur Aboud amezungumza na katibu mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ya Tanzania, Bi. Mariam J Mwaffisi, na kwanza anazungumzia matokeo ya mkutano wao.