Majeshi ya UM yachukua udhibiti huko Chad kutoka kwa kikosi cha EU

16 Machi 2009

Walinda amani wa UM huko Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati walichukua udhibiti wa kijeshi na usalama kutoka kwa kikosi cha Ulaya katika mataifa mawili hayo yenye kukumbwa na ghasia.

Sherehe za kukabidhi mamlaka ya maeneo hayo yalifanyika katika mji wa mashariki mwa Chad wa Abeche na kuhudhuriwa na naibu katibu mkuu wa shughuli za kulinda amani Alain Le Roy. Mwezi Januari Baraza la Usalama liliidhinisha kupelekwa zaidi ya wanajeshi elfu 5 500 wakulinda amani, polisi 300, wanafanyakazi wa kijeshi 5 200, kutumikia ofisi ya UM huko kuchukua nafasi ya wanajeshi wa Ulaya walopelekwa huko tangu mwezi Marchi mwaka jana. Taarifa ya KM iliyotolewa na msemaji wake inapongeza kazi za wanajeshi wa Ulaya kuwalinda watu walopoteza makazi yao, wakimbizi na wakazi huko mashariki ya Chad na kaskazini mashariki ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter