Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waathiriwa wa vita wanahitaji kupata maji masafi na usafi

Waathiriwa wa vita wanahitaji kupata maji masafi na usafi

Kamati ya kimataifa ya Msalaba Mwekundu ICRC, imesema ni lazima kwa jumuia ya kimataifa kufanya kazi zaidi kuhakikisha kwamba waathiriwa wa vita wanapata maji masafi na huduma za usafi.

Mkuu wa Idara ya Maji na Usafi ya ICRC, Robert Mardini alitoa mwito huo kwa wajumbe wa serekali zinazoshiriki katika mkutano wa 5 wa maji duniani huko Istambul Uturuki. Kamati hiyo imesisistiza kwamba huduma za maji, usafi na umeme pamoja na vituo vya afya ni mambo yanayo haribiwa kwanza vita vikizuka. Bw Mardini alitaja Iraq, Gaza, Sri Lanka na Somalia kama mfano ambako huduma za maji na usafi ziliathiriwa sana akisema ukosefu wa huduma hizo kunaweza kusababisha kuenea kwa haraka sana magonjwa.