Ripoti ya UM juu ya hali ya misitu duniani

Ripoti ya UM juu ya hali ya misitu duniani

Changamoto kutokana na mzozo wa kiuchumi na mabadiliko ya hali ya hewa, zimeleta kwenye mstari wa mbele usimamizi wa misitu miongoni mwa watalamu wa dunia.

Ripoti mpya ya UM juu ya hali ya misitu duniani iliyotolewa wakati wa mkutano wa Idara ya Chakula na Kilimo FAO, juu ya misitu, huko Roma inaeleza wasi wasi kwamba kutokana na mzozo wa kiuchumi serekali za dunia huwenda zisitiliye mkazo tena juu ya mapinduzi ya kijani, ikiwa ni kuongeza juhudi za kupanda miti na usimamizi bira zaidi wa misitu. Inasema kuzidi kwa mzozo wa kiuchumi kutasababisha watu kutafuta zaidi kuni kama njia ya nishati na hivyo kuhatarisha zaidi misitu.