Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Mkutano wa tano wa maji duniani ulifunguliwa Jumatatu mjini Istambul, Uturuki ukiwa na lengo la kuliweka suala la maji katika ajenda ya kimataifa.

UM umetoa mwito wa kuwepo na usimamizi bora zaidi ili kukabiliana na upungufu wa maji duniani. Mkurugenzi mkuu wa UNESCO, Koichiro Matsuura anasema wakati mahitaji ya maji masafi yanaongezeka duniani huduma za maji na usafi zinaendelea kua chache katika nchi zinazoendelea. Alisema, kupambana na umaskini kunategemea uwezo wa kuwekeza katika usimamizi wa maji.

Ujumbe wa Baraza la Usalama umekamilisha ziara yake ya siku nne Haiti ya majadiliano juu ya masuala ya usalama na amani, pamoja na maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Kabla ya kuondoka ujumbe huo mwiswhoni mwa wiki ulishiriki katika kufunguliwa upya chuo cha wanasheria, huko Port-au-Prince, ikiwa hatua muhimu kabisa ya mageuzi ya mfumo wa sheria nchini Haiti.

Rais Hamid Karzai alizindua kampeni ya mpango unao ungwa mkono na UM wa kuwachanja watoto karibu milioni 7.7 huko Afghanistan, pamoja na India, Pakistan na Nigeria, ambako ugonjwa huo bado ni sugu. Rais Karzai alitoa chanjo kwa watoto katika ikulu, kuanzisha kampeni ya siku tatu itakayofanyika katika majimbo 34 ya Afghanistan, ikisimamiwa na wizara ya afya ikisaidiwa na shirika la watoto la UM UNICEF na shirika la afya duniani WHO.

UM umetangaza kwamba wafanyakazi wake walotekwa nyara huko Somalia Jumatatu asubuhi, waliachiliwa huru saa nne kasoro dakiki ishirini saa za Somalia kwa walinzi wa UM. Wafanyakazi hao walitekwa nyara na watu wasojulika walipokua wanaelekea uwanja wa ndege katika mji wa Waajid, kati kati ya Somalia.