Kikao cha Kamisheni juu ya Hali ya Wanawake
Leo hii, tunazungumzia juu ya Kikao cha 53 cha Kamisheni juu ya Hali ya Wanawake, kinacho malizika katika makao makuu ya UM Ijumaa tarehe 13.
Wajumbe kwenye mkutano huo walisisitiza tena, juu ya haja ya wanawake na wanaume kufanya kazi pamoja katika majukumu ya malezi, kuwahudumia waathiriwa wa HIV na Ukimwi, pamoja na majukumu ya nyumbani. Wajumbe pia walizungumzia juu ya mafanikio tangu mkutano mkuu juu ya wanawake huko Bejing. Abdushakur Aboud amezungumza na mmoja wapo wa wajumbe kutoka JKK Rosette Saiba Lwanzo, naibu mjumbe wa utawala katika idara ya utali, akizungumzia zaidi juu ya utumiaji nguvu dhidi ya wanawake