Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Ripoti mpya ya UM inaonya kwamba kuongezeka haraka idadi ya wakazi duniani, mabadiliko ya hali ya hewa, uwongozi mbaya wa matumizi ya rasilmali na kuongezeka kwa mahitaji ya nishati, kumezidisha mahitaji ya maji yanayokauka haraka duniani.

KM Ban Ki-moon na Rais Barack Obama wa Marekani wamesisitiza haja ya mwaka 2009 kua mwaka wa mabadiliko ya hali ya hewa, wakati mataifa ya dunia yanajitayarisha kukamilisha mazungumzo juu ya mkataba mpya wa kupunguza gesi za sumu za greenhouse. Katika mkutano wake wa kila mwezi na waandishi habari hapa katika makao makuu, Bw Ban alisema alipokutana na kiongozi wa Marekani mapema wiki hii, walikubaliana kwamba mabadiliko ya hali ya hewa yanasbabisha kitisho muhimu, na wamenuia kuufanya mwaka 2009 kua ni wa kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Mtaalamu huru wa UM anaehusika na watu walokimbia makazi yao IDP's, Walter Kaelin, ametoa mwito kwa watu kushughulikia zaidi baadhi ya matatizo makubwa ya mzozo wa walokimbia makazi yao duniani, ikiwa ni pamoja na yale yanayotokana na ajali za kimaumbile na vita huko Somalia, Sri Lanka na Sudan. Bw Kaelin amasema zaidi ya watu milioni 26 kote duniani wamepoteza makazi yao kutokana na vita na ghasia. Amesema kuna haja ya dharura kwa jumuia ya kimataifa kushughulikia zaidi baadhi ya mizozo mibaya kabisa duniani.

Mjumbe maalum wa UM kwa ajili ya Somalia Ahmedou Ould-Abdallah ameipongeza serekali mpya ya Somalia kwa maendeleo iliyoweza kufanya mnamo mwezi uliyopita na kuihimiza kufanya kazi kuelekea amani na uthabiti. Katika taarifa yake iliyotolewa Nairobi, mjumbe maalum amewahimiza wa-Somali na jumuia ya kimataifa kuisaidia serekali hiyo mpya katika kuleta amani na utulivu. Bw Ould-Abdallah amesema ameridhika na idadi fulani ya "wabunge wazalendo" walorudi Mogadishu na kuanza kazi zao, akitoa mwito wakutolewa msaada wa dhati wa kidiplomasia na rasilmali kusaidia vyombo viwili vya utawala nchini humo.