Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM ahimiza majadiliano Madagascar mzozo ukizorota

KM ahimiza majadiliano Madagascar mzozo ukizorota

KM Ban Ki-moon alitoa mwito wa kuwepo majadiliano kati ya viongozi wa pande zote huko Madagascar, wakati mvutanowa kisiasa unazidi kuzorota na wasi wasi kuongezeka juu ya kugawika kwa jeshi.

Taarifa ya KM iliyotolewa jana, inarudia kusisitiza kwamba suluhisho pekee kwa mzozo wa sasa ni kuanza tena mazungumzo na alitoa mwito kwa pande zote kutekeleza ahadi zao za kutanzua tofauti kati yao kufuatana na misingi ya kuitisha Mkutano wa Kitaifa. Rais Marc Ravalomanana na meya wa Antananarivo, Andry Rajoelina walitangaza mwezi uliyopita wanania ya kuanza majadiliano yatakayosimamiwa na UM. Karibu watu 135 wameuliwa tangu mwezi Januari katika ghasia zilizozuka kutokana na ugomvi huo wa kisiasa.