Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM na AU kupambana pamoja dhidi ya uhalifu na madawa ya kulevya

UM na AU kupambana pamoja dhidi ya uhalifu na madawa ya kulevya

Idara ya UM ya kupambana na uhalifu na Umoja wa Afrika AU, walizindua mpango wa pamoja kusaidia mradi wa miaka mitano ijayo, wa nchi za ki-Afrika kupambana na biashara haramu inayopanuka ya madawa ya kulevya na shughuli za uhalifu zinazoambatana na biashara hiyo barani humo.

Mpango huo wa pamoja wa UM na AU ulozinduliwa huko Vienna, siku ya Alhamisi, unalengo la kuimarisha uwezo wa tume ya AU na mashirika ya kikanda, hasa Jumuia ya Uchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi ECOWAS, kuweza miongoni mwa mambo mengine kupanga sera, na kuwafundisha waatalamu katika kila kiwango wa tatizo hilo. Afisi ya UM ya kupambana na madawa ya kulevya na uhalifu UNODC inaeleza kwamba jumuia ya kimataifa ina wasi wasi kutokana na kuongezeka utumiaji wa Afrika ya Magharibi kama kituo cha muda kupitisha madawa ya kulevya kuelekea Ulaya kutoka Amerika ya Kusini, kutokana na ukosefu wa ulinzi wa mipaka na taasisi dhaifu za usalama na za ki-taifa katika kanda hiyo ya Afrika.