Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haja ya kurahisisha zaidi wagonjwa wa UKIMWI kupata madawa ya ARV's

Haja ya kurahisisha zaidi wagonjwa wa UKIMWI kupata madawa ya ARV's

Mkurugenzi mkuu mpya wa shirika la kupambana na Ukimwi la UM UNAIDS, anasema kuna haja ya kuimarisha huduma za kutibu HIV, ikiwa njia muhimu ya kupunguza uwambukizaji wa virusi kutoka kwa mama hadi mtoto.

 Akizungumza na waandishi habari mjini Geneva Michel Sidibe, alifafanua kile anachodhani ni vipaumbele vya UNAIDS katika miaka inayokuja. Alisema ni muhimu kuongeza juhudi za kupunguza uambukizaji mpya, kwani kila mtu mmoja akipewa matibabu kuna wengine watatu wepya wana ambukizwa. Kiasi ya dola bilioni 14 zilitumiwa kupambana na ukimwi mwaka jana, lakini ni kiasi ya asili mia 30 hadi 35 ya watu walohitaji matibabu waloweza kuyapata. UNAIDS inakadiria kwamba ifikapo 2011 kiasi ya watu milioni 14 watahitaji matibabu, na kwa wakati huu kuna milioni 6 hawapati matibabu, hiyo ikiwa ni changamoto kubwa inayobidi kukabiliwa.