Wasi wasi wazidi huko Madagascar baada ya mkutano kutofanyika tena

12 Machi 2009

Mkutano ulopangwa kufanyika kati ya pande zinazogombana huko Madagascar haukuweza kufanyika tena hii leo baada ya meya wa Antananarivo, Andry Rajoelina kukata kuhudhuria mazungumzo.

Akizungumza na Redio ya UM naibu katibu mkuu wa masuala ya kisasa Haile Menkeriou, anasema hali ni ya wasi wasi hasa kufuatia mabadiliko yaliyofanyika katika jeshi wiki hii.

"Kilichotokea jana na juzi ndani ya jeshi kimesababisha mabadiliko ya misimamo katika pande zote mbili. Kundi la meya na wafuasi wake wametiwa moyo na jinsi maafisa wa vyeo vya chini wanavyo waunga mkono na kuipinga serekali".

Menkerios ameonya pande zote mbili kutovutana hadi kusababisha jeshi kuweza kuingilia kati na kuchukua madaraka. Anasema za UM ni kuhakikisha majadiliano yanaendelea hadi kupatikana suluihisho kwa njia ya amani. Anasema Meya Rajoelina, amefafanua bayana kasoro za uwongozi wa rais Marc Ravalomanana, lakini hajasema kwa upande wake kile anachotaka kufanya.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter