Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM Ban ana wasi wasi kutokana na kutekwa wafanyakazi wa msaada Darfur

KM Ban ana wasi wasi kutokana na kutekwa wafanyakazi wa msaada Darfur

KM Ban Ki-moon ameeleza wasi wasi wake hii leo kutokana na kutekewa nyara wafanyakazi watatu wa huduma za dharura huko Darfur, na kwa mara nyingine tena alitoa mwito kwa Serekali ya Sudan kubadili uwamuzi wake wa wiki iliyopita, wa kuyafukuza makundi 13 muhimu ya misaada.

Wafanyakazi hao watatu walotekwa nyara Ijumatano wanafanya kazi na kundi la Madaktari wasio na Mpaka MSF lenye makazi yake Ubelgiji. Akizungumza na waandishi habari mjini New York, Bw Ban alisisitiza kwamba makundi haya yana jukumu muhimu sana katika kuwasaidia kiasi ya watu milioni 4.7 katika jimbo hilo la magharibi lenye ghasia. Alisema wasi wasi mkubwa wa UM huko Sudan, daima imekua na itaendelea kua ni kuleta amani na usalama wa wananchi wa taifa hilo.