Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo kuzihusisha pande zote Afrika ya Kati kutapelekea amani

Mazungumzo kuzihusisha pande zote Afrika ya Kati kutapelekea amani

Mjumbe Maalum wa KM kwa ajili ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, ameliambia Baraza la Usalama kwamba mazungumzo yaliyokua yanasubiriwa kwa muda mrefu ya vyama vyote yameweza kuleta nafasi ya kupiga hatua kuelekea amani ya kudumu katika nchi hiyo isiyopakana na bahari.

Alisema mazungumzo yaliyofanikiwa mwezi wa Disemba katika mji mkuu wa Bangui ni matokeo ya juhudi za miaka miwili ya watu mbalimbali wa kitaifa kutoka serekali, upinzani, mashirika yasiyo ya kiserekali na jumuia ya kimataifa. Ameliambia baraza kwamba baada ya mkutano huo wa siku 12, makubaliano kadhaa yalifikiwa ikiwa ni pamoja na kuundwa serekali ya mseto ya pande zote, ahadi ya kuitisha uchaguzi mwaka huu na mwakani na kuundwa kamati huru ya uchaguzi.