Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Akizungumza na kamati ya masuala ya kigeni ya bunge la Marekani KM Ban Ki-moon aliwakumbusha wabunge kwamba Marekani baado inadaiwa dola bilioni moja na Umoja huo, akisema hawawezi kufanya kazi wanaombiwa kufanya bila ya rasilmali inayohitajika.

Masuala mengine yaliyojadiliwa ni Afghanistan, Haiti, Sudan, Ghaza, Somalia na Mabadiliko ya Hali ya Hewa.

Kiasi ya afisa 332 wa Kongo walomaliza mafunzo yao katika mji wa Kisangani wanapelekwa kusaidia kulinda afisi za UM MONUC na ya miradi nchini humo UNOPS. Askari 60 watalinda mradi mkubwa wa ujenzi wa barabara kati ya Sake na Masisi, ambako kuna wafanyakazi 1200. Mjumbe Maalum wa KM Alan Doss aliwaambia waandishi habari kwamba kuna kazi kubwa ya kufanywa kwa upande wa huduma za dharura ingawa kumepatikana amani hivi karibuni huko Mashariki ya JKK.

Akifungua maonesho ya utali ya Berlin Mkurugenzi wa Shirika la UM la Utali UNWTO, Taleb Rifai, amesema sekta hiyo ya safari za mapumziko inabidi kua sehemu muhimu kabisa katika lengo la kubadilisha kuduma kwa uchumi duniani. Amesema Utali una maana ya biashara, ajira, maendeleo, utamaduni amani na kutekelezwa ndoto za binadamu.

Fuko la Kimataifa la Global Fund, limepongeza tangazo la bunge la Marekani kutoa msaada wa karibu dola milioni 900 kwa ajili ya fuko hilo la kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria. Msaada huo wa Marekani ni mkubwa kuwahi kutolewa kwa fuko hilo, na Mkurugenzi Mkuu wake Michel Kazatchkine anasema hiyo ni ishara muhimu ya kupambanana magonjwa ya kuambukizwa inayotolewa na bunge la Marekani.