Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Idara ya UM ya kupambana na mabomu yaliyotegwa ardhini, UNMAS imetangaza kwamba serekali ya Japan itatowa karibu dola milioni 7.7 ya msaada kwa ajili ya juhudi za kuondowa mabomu yaliyotegwa ardhini huko JKK na Chad.

Mkurugenzi wa UNMAS Max Kerley alisema huu ni msaada mkubwa utakaosaidia kuimarisha hali ya maisha ya mamia ya watu wanapokabiliwa na hatari ya kila siku kutokana na mabomu hayo, ambayo hayajaripuka na yaliyotegwa miaka mingi sasa.

Mjumbe maalum wa KM Ban Ki-moon huko JKK Alan Doss amesema mwito wa kuwataka waasi wa Kinyarwanda huko mashariki ya Kongo kurudi nyumbani unaleta matokeo mazuri kwa amani na usalama katika eneo hilo lililokumbwa na vita. Bw Doss amesema, wapiganaji wa kundi la wanamgambo la FDLR wamekua pia wakiasalimisha silaha zao pole pole, akiongeza kusema huu ni ushahidi kwamba ujumbe wao wa kuweka chini silaha na kurudi nyumbani kwa heshima, unaitikiwa.

UM unahusika kwa karibu sana katika juhudi za kutanzua mzozo wa kisiasa huko Madagascar kwa njia ya amani amesema Marie Okabe, msemaji wa Umoja huo. Amesema UM unafanyakazi kwa pamoja na jumuia ya kimataifa pamoja na kusaidia juhudi zote za pamoja kuhakikisha usalama wa raia, wakati wanatafuta suluhisho kwa mozoz huo. Naibu KM Haile Menkerios, aliyepelekwa huko alisema pande zinazo gombana zimekubaliana juu ya awamu mbili za mazungumzo kuweza kutanzua matatizo yao.