Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuporomoka kwa biashara duniani kunaweza kuathiri zaidi wanawake

Kuporomoka kwa biashara duniani kunaweza kuathiri zaidi wanawake

Akifungua mkutano juu ya "umuhimu wa jinsia katika biashara" mkurugenzi mkuu wa shirika la Biashara Duniani UNCTAD Bw Supachai Panitchpakdi amezipendekeza serekali zinazo tayarisha mipango ya kujaribu kuufufua uchumi ili kukabiliana na mzozo wa kifedha duniani kufikiria juu ya kuweka hatua za kuimarisha ajira kwa ajili ya wanawake na kusaidia biashara ndogo ndogo zinazoendeshwa na wanawake.

 Waatalamu kwenye mkutano huo, uloanza iJumanne, wameonya kwamba kuporomoka kwa biashara kufuatia mzozo wa kiuchumi duniani huwenda kukawaathiri zaidi nafasi za kazi za wanawake wengi katika nchi zinazoendelea. UNCTAD inakadiria kwamba kiwango cha bidhaa zinazosafirishwa nje kutoka nchi zinazoendelea huwenda kikashuka kwa asili mia 15.5 mwaka 2009. Makadirio ambayo Bw Supachai anasema, huwenda yakawa ni mazuri, lakini hata hivyo anadokeza kwamba wanawake wamekua mstari wa mbele katika baadhi ya sekta muhimu za bidhaa zinazosafirishwa nje katika nchi zinaozendelea, na ajira zilongezeka haraka wakati wa hali nzuri. Hivyo anasema hivi sasa kushuka kwa biashara, wanawake wengi watapoteza ajira hizo na amezitaka serekali kutilia mkazo maslahi ya wanawake katika miradi yao mipya ya kufufua uchumi.