Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nafasi milioni 10 zaweza kubuniwa kwa kukuza misitu

Nafasi milioni 10 zaweza kubuniwa kwa kukuza misitu

Naibu mkurugenzi wa shirika la Chakula na Kilimo Duniani FAO amesema, wakati nafasi zaidi za ajira zinapotea kutokana na kuendelea kuzorota hali ya uchumi, kuna uwezekano wa kubuni mamilioni ya nafasi za kazi za kijani, kwa kuwepo na usimamizi bora wa misitu.

 Bw Jan Heino wa Idara ya Misitu ya FAO amesema, usimamizi mzuri wa misitu utasaidia kupunguza umaskini na kuimarisha mazingira, kwa vile misitu na miti ni muhimu kabisa kuvuta gesi ya carbon, na hivyo uwekezaji huo unaweza kuchangia sana katika mabadiliko ya hali ya hewa. Kufuatana na utafiti wa hivi karibuni wa Shirika la Kazi Duniani ILO, kiwango cha wasokua na kazi duniani kimeongezeka kutokea milioni 179 kwa mwaka 2007 na kufikia milioni 198 mwaka 2009 na hata kuweza kufikia milioni 230 mambo yakizidi kua mabaya. Suala la jinsi usimamizi thabiti wa misitu linavyoweza kujenga mustakbal wa kijani na kukidhi mahitaji ya jami ya bidhaa na huduma kutokana na msitu litakua kiini cha mkutano wa kamati ya misitu ya FAO huko Rome kuanzia March 16 hadi Marchi 20