Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mauwaji ya wanaharakati wa haki za binadamu Kenya

Mauwaji ya wanaharakati wa haki za binadamu Kenya

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu Bi Navi Pillay, ametoa mwito wa uchunguzi kufanyika baada ya muasisi wa kundi la kutetea haki za binadamu kuuliwa mjini Nairobi siku ya Alhamisi, wakati wa magharibi.

Bi Pillay alitoa mwito huo baada ya kukutana na Mjumbe Maalum wa UM kwa ajili ya mauwaji ya kiholela. Profesa Philip Alston, ambae wiki iliyopita alitoa taarifa inayoeleza kwamba polisi wa Kenya "wanapanga kwa makini na kufanya mauwaji ya kiholela bila ya kuwajibika dhidi ya kundi lililopigwa marufuku la Mungiki".

Muasisi wa kundi la Oscar Foundation, Oscar Kamau Kingara aliuliwa pamoja na mshauri wake wa habari John Paul Oulu wakiwa garini karibu na Chuo Kikuu cha Nairobi wakielekea kwenye mkutano na maafisa wa Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu ya Kenya KNCHR. Naibu mwenyekiti wa tume hiyo, Hassan Omar anasema wamelaani mauwaji hayo ya kikatili na kutaka uchunguzi kamili ufanyika.

HASSAN OMAR

Akizungumza na redio ya UM Mjumbe Maalum kwa ajili ya mauwaji ya kiholela, Profesa Alston anasema wakati wa ziara ya hivi karibuni huko Kenya alikutana na wanaharakati hao wawili amabo walikua wanatoa msaada wa bure wa masuala ya kisheria na haki za binadam kwa wa Kenya. Na hapo, mwaka 2007 walitoa ripoti kamili ya kuhusika polisi katika mauwaji ya kiholela, na walimpa ushahidi wa kutosha juu ya matukiyo hayo. Amesema cha kusikitisha ni kwamba kila ishara inaonesha polisi walihusika na muawji hayo.

Anasema cha muhimu hivi sasa kuna tuhuma zinazo tolewa dhidi ya polisi, hivyo basi changa moto ni juu yao kujisafisha. Na njia pekee kufanya hivyo anasema ni kuitisha uchunguzi huru kutoka njee kama vile Afrika Kusini.

Bw Alston anasema hadi hivi sasa serekali ya Kenya haijasema lolote kuhusu ripoti yake juu ya tuhuma za mauwaji ya kiholele na kuitaka serekali kuwafukuza kazi mkuu wa polisi na mwanasheria mkuu wa nchi. Anasema cha kukera ni kwamba kundi la Mungiki kinachotuhumiwa kwa tabia za uhalifu kilitisha mandamano mapema wiki hii. Na lengo la maandamano hayo ni kumulika ripoti na mapendekezo yake. 

Anasema, lakini kwa bahati mbaya mandamano hayo yameleta athari mabya kwani imewapatia polisi nafasi ya kulalamika tena juu ya shughuli za kihalifu za kundi hilo na hapo kunaza msako wake na matokeo ni mauwaji ya wanahaakati hao.

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu ameihimiza serekali ya Kenya kuhakikisha usalama kwa mashahidi wa mauwaji hayo, kufanya uchunguzi na kuwafikisha wahalifu mahakamani.

Ni hayo tukliyokua nayo hii leo kwa niaba ya Abdushakur Aboud ni mimi AK na fundi wa mitambo Carlos kutoka studio za Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya UM, New York tunasema kwaherini.