Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IAEA kutumia teknolojia ya nuklia kupambana na ndorobo

IAEA kutumia teknolojia ya nuklia kupambana na ndorobo

Wanasayansi wa idara ya Kimataifa ya Nishati ya Atomiki IAEA wanatayarisha mpango wa kudhibiti nzi wenye wa hatari wa aina ya ndorobo, kwa kutumia teknolojia ya nuklia.

 Ndorobo wanapatikana katika mataifa 37 ya Afrika na hubeba vijidudu vinavyosababisha ugonjwa wa kuharisha miongoni mwa mifugo na ugonjwa wa malale mionogoni mwa binadamu, ugonjwa ambao unaweza kusababisha kifo usipotibiwa. Kufuatana na shirika la Afya Duniani watu milioni 60 wanaoishi mashambani huko Afrika mashariki, kati na magharibi wako hatarini ya kuambukizwa na ugonjwa wa malale.