Alston atoa mwito wa uchunguzi kutokana kuuliwa wanaharakati wa Haki za Binadamu Kenya

6 Machi 2009

Mtaalamu maalum wa UM kuhusiana na mauwaji ya kiholela Profesa Philip Alston ametoa mwito wa uchunguzi wa kina kufanyika kutokana na kuuliwa kwa wanaharakati wawili wa kutetea haki za binadama huko Kenya.

Washambulizi wasojulikana waliwauwa jana magharibi, mkurugenzi mwanzilishi wa kundi la kutetea haki za binadamu Oscar Foundation, Oscar Kamau Kingara na mshauri wake wa mawasiliano John Paul Oulu, walipokua wanaelekea kuhudhuria mkutano na maafisa wa Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu ya Kenya. Akizungumza na redio ya UM Prof Alston alisema ni jambo la kukera kabisa kuona mtu anaefanyakazi kutetea haki za binadamu anaweza kuuliwa hadharani, mchana mjini Nairobi. Alisema kitendo hicho ni tishio kubwa kwa utawala wa kisheria, bila ya kujali aliyewajibika na mauwaji hayo. Nae naibu mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu ya Kenya Hassan Omar, anasema hicho ni kitendo cha kukera na watu wengi wanadhani polisi walihusika na mauwaji hayo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter