Rais wa Baraza Kuu kulaani kufunguliwa mashtaka Bashir

5 Machi 2009

Rais wa Baraza Kuu la UM Balozi Miguel d\'Escoto Brockman, akizungumza na waandishi habari mjini Geneva amesema UM haujatengwa kutokana na kundi la mataifa tajiri na yanayoinukia G20 yanakutana kando.

Alisema njia ya kutanzua mzozo wasasa ni kuwepo na mageuzi makubwa ya karne ya 21 kwa mataifa yote 192 ya UM. Wakati huo huo balozi Brockman amelaani kufungiliwa mashataka Rais Omar Al-Bashir wa Sudan na ICC, akisema ni pigo kwa haki za kimataifa kwa utawala wa kisheria. Anasema anadhani ni jambo la kusikitisha hatua hiyo kuchukuliwa licha ya mwito wa Umoja wa Afrika AU na Umoja wa nchi za Kiarabu kwa Baraza la Usalama kupatia amani kipaumbele huko Sudan, na kusitisha kutolewa hati ya kukamatwa kwa Bw Bashiri kwa mwaka mmoja.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter