Libya itazingatia sera ya kulinda amani na Sudan wakati inaongoza Baraza la Usalama

4 Machi 2009

Libya inasema miongoni mwa masuala itazingatia mnamo mwezi huo inaposhikilia uwenyekiti wa Baraza la Usalama la UM ni sera ya kazi za kulinda amani na athari zinazoweza kutokea, kutokana na uwamuzi wa Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa kutoa kibali cha kukamatwa kwa Rais wa Sudan.

Balozi wa Libya Ibrahim Dabbashi, akizungumza kabla ya uwamuzi kutolewa amesema hakuna kikao maalum kilichopangwa kulijadili suala hilo hata hivyo amesema mashauriano kati ya wanachama wa baraza yanaendelea juu ya uwezekano wa kutumia kifungu cha 16 cha mkataba wa Rome uloanzisha ICC, kitakacho chelewesha uchunguzi kuhusiana na mashataka hayo kwa miezi 12. Alisema ni muhimu Baraza la Usalama litafakari suala hilo kuambatana na maamuzi yatakayochukuliwa na mashirika ya kikanda hasa Umoja wa Afrika na Umoja wa Nchi za Kiarabu.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter