Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICC yatoa hati ya kukamatwa Rais wa Sudan kwa uhalifu wa vita Darfur

ICC yatoa hati ya kukamatwa Rais wa Sudan kwa uhalifu wa vita Darfur

Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa ICC imetoa hii leo hati ya kukamtwa Rais Omar Al-Bashir kwa mashtaka ya uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya ubinadamu ulotendeka katika jimbo linalokumbwa na ghasia la Darfur.

null

Hii ni mara ya kwanza kwa mahakama hiyo kumfungulia mashtaka mkuu wa taifa akiwa madarakani. Katibu mkuu wa UM Ban Ki-moon alitoa taarifa hii leo akisema ana imani kwamba serekali ya Sudan itaendelea na utaratibu wa kuhakikisha amani na usalama kuambatana na azimio nambari 1593 la Baraza la Usalama. Amesema UM utaendelea kufanya kazi zake muhimu za kulinda amani, huduma za dharura, haki za huduma za kibinadam na maendeleo huko Sudan. Bw Ban alitoa mwito kwa serekali ya Khartoum kushirikiana kikamilifu na mashirika yote ya UM na washirika wake kwa kutekeleza majukumu yake kuhakikisha usalama wa raia, wafanyakazi wa UM na mali zao pamoja na washirika wao. Al-Bashir ameshtakiwa kwa makosa mawili ya uhalifu wa vita na makosa matano ya uhalifu dhidi ya ubinadam. Hata hivyo mahakimu wa mahakama ya The Hauge walosikiliza kesi ya awali walisema hapakua na ushahidi wa kutosha kumshitaki kwa mauwji ya kimbari, lakini walisisitiza kwamba ikiwa mwendesha mashtaka atawasilisha ushahidi zaidi wataweza kubadilisha mashtaka. Inakadiriwa watu laki tatu wamefariki huko Darfur katika kipindi cha miaka mitano ya ghasia kati ya waasi na wanajeshi wa serekali pamoja na washirika wao wanamgambo wa kundi la Janjaweed. Mahakimu wakitoa uwamuzi wao wamesema kwa vile Al-Bashir alikua rais wa Sudan na kamanda mkuu wa majeshi, anatuhumiwa kwa kuratibu, kupanga na kutekeleza kampeni ya kupambana na uwasi.