Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Naibu katibu mkuu wa UM Asha-Rose Migiro amehimiza hatua za haraka kuchukuliwa kunganisha idara zote za UM zinazohusiana na masuala ya wanawake ili kuimarisha juhudi za kufikia usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake kisasa, kiuchumi na kijami.

Akizungumza kwenye mkutano wa mawaziri wa masuala ya wanawake, wanaohudhuria kikao cha 53 cha Kamisheni ya hali ya Wanawake mjini New York, Bi Migiro alisema kwa wakati huu kuna idara nne zinazoshughulikia masuala ya wanawake na wakati umefika kuunda idara moja ya usawa wa kijinsia. 

Kufuatia uwamuzi wa Mahakama ya Uhalifu wa kimataifa ICC ya kutoa hati ya kukamatwa kwa Rais Omar Al-Bashir, hapakua na ripoti za ghasia huko Sudan, bali kumekuwepo na maandamno ya amani mjini Khartoum kupinga uwamuzi huo. Kulikuwepo pia na maandamano ya amani katika miji ya Darfur ya Magharibi na maandamano mengine yamepangwa Alhamisi kuunga mkono uwamuzi huo alisema Msemaji wa KM Michele Montas. UNAMID imeripoti kwamba polisi na walinda amani waliendelea na kazi zao za kawaida za kupiga doria, na kufuatilia kwa makini hali ya mambo.

Afisi ya kulinda amani ya UM huko JKK, MONUC, imeweza kuwapokonya silaha watoto 880 walokua wameandikishwa na makundi ya kivita katika jimbo lenye ghasia la mashariki la Kivu ya Kaskazini kati ya Januari 30 hadi March pili. Msemaji wa MONUC Madnodje Mounoubai amesema watoto wote wamekabidhiwa makundi yasiyo ya kiserekali ili kuwarudisha na kujiunga tena na familia na jamii zao.