Mkuu wa Mazingira kuongoza Makao Makuu ya UM Nairobi

3 Machi 2009

KM Ban Ki-moon amemteua mkuu wa Shirika la Mazingira la UM, UNEP kua mkurugenzi mkuu wa Makao Makuu ya UM huko Nairobi. Achim Steiner aliyeanza awamu ya miaka minne kuiongoza UNEP 2006, ataendelea kua mkuu wa shirika hilo na kuchukua nafasi iliyokua inashikiliwa na Bi Anna Tibaijuka, ambae ataendelea kua mkurugenzi mkuu wa Shirika la Makazi UN-HABITAT. Msemaji wa KM amesema uwamuzi huo ulichukuliwa kufuatana na sera za Bw Ban za kuwabadilisha kwa zamu wakurugenzi wakuu wa mashirika ya UM.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter