Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM unaeleza kua mzozo wa kifedha utazidisha umaskini

UM unaeleza kua mzozo wa kifedha utazidisha umaskini

Utafiti mpya wa Umoja Ma mataifa unaeleza kwamba mzozo wa kifedha duniani unaokumba masoko ya fedha ya Marekani na Ulaya utawathiri watu fukara duniani na kuwatumbukiza mamilioni katika umaskini zaidi na kupelekea vifo vya maelfu ya watoto.

Kupunguka ukuwaji kwa 2009 kutagharimu watu milioni 390 wa Afrika wanaoishi katika umaskini kabisa, kiasi ya dola bilioni 18, ikiwa ni kupungukiwa kwa asili mia 20 ya mapato yao. Utafiti huo ulotayarishwa na idara ya Elimu kwa Wote Duniani ya shirika la UM la Elimu na Sayansi, UNESCO, ulikua na lengo la kutathmini athari za mzozo wasasa wa fedha na uchumi duniani katika ushrikiano wa kimataifa kwa ujumla na kwa elimu, sayansi, utamaduni, habari na mawasiliano. Ripoti hiyo inasisitiza juu ya kuongezeka kwa kati ya vifo laki mbili hadi laki nne ya watoto wachanga na utapiamlo, ambao tayari unaongezeka na utakua sababu kuu ya vifo miongoni mwa watoto.