Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Mkuu wa Idara ya Kazi za kulinda amani za UM Alan Le Roy, amesema amehakikishiwa kwamba kikosi cha pamoja cha UM na Umoja wa Afrika huko Darfur UNAMID, hakita kabiliwa na kitisho ikiwa mahakama ya uhalifu ya kimataifa itatoa kibali cha kukamatwa Rais Omar Al-Bashir.

 Akizungumza kwenye makao makuu ya UM Bw Le Roy alisema serekali itatekeleza wajibu wake kamili wa kulinda afisi zote za UM huko Sudan dhidi ya athari zozote mbaya kutokana na uwamuzi wa ICC.

KM wa UM Ban Ki-moon amelaani vikali mauwaji ya rais wa Guinea Bissau Joao Bernardo Vieira na mkuu wake wa majeshi, akitoa mwito kwa mamlaka ya usalama nchini humo kudumisha utawal wa sheria na kuwafikisha mahakamani walohusika. Taarifa ya KM inaeleza kwamba, anawasiliana na mwakilishi wake huko Guinea Bisaau ambae anashirikiana na jumuia ya kimataifa huko kuhamasisha amani utulivu wa kisiasa na maendeleo katika nchi hiyo.

Akikifungua kikao cha 53 cha kamiksheni ya UM juu ya hali ya wanawake, naibu katibu mkuu Asha-Rose Migiro alisema wanawake wengi sana wanabeba jukumu zito kabisa la kuwahudumia watu wanaoishi na virusi vya HIV na Ukimwi, akitoa mwito wa kuwepo usawa zaidi katika majukumu kati ya wanaume na wanawake. Alisisitiza kwamba janga la VVU/Ukimwi linaashiria haja ya kuchukuliwa mkakati jumla wa kumhusisha kila mtu katika jamii kukabiliana na hali hiyo ya ukosefu wa usawa.

KM Ban Ki-mmon amesifu juhudi kabambe zilizochukuliwa mnamo miaka 10 iliyopita kuondowa mabomu yaliyotegwa ardhini kote duniani, akisisitiza kwamba kungali na kazi kubwa kutokomeza silaha hiyo ya hatari. Katika taarifa ya KM ilitolewa kuadhimisha miaka 10 tangu kuanza kutekelezwa Mkataba wa kupiga marufuku mabomu ya kutegwa ardhini, inasistiza kwamba mafanikio yaliyopatikana ni makubwa na yanaonekana.