Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya hali ya hewa kuweza kuathiri sana uvuvi duniani

Mabadiliko ya hali ya hewa kuweza kuathiri sana uvuvi duniani

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo limechapisha ripoti hii leo ikionya kwamba ni lazima biashara ya uvuvi na idara za kitaifa za uvuvi zichukuwe hatua zaidi kufahamu na kujitayarisha kutokana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa uvuvi duniani.

Kufuatana na ripoti hiyo ya FAO tabia bora za uvuvi zitekelezwa kwa maeneo mengi zaidi na mipango ya sasa ya kuendesha biashara inabidi kupanuliwa ikiwa ni pamoja na kutayarisha mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Ripoti ina sisitiza juu ya haja ya kusaidia jamii zinazotegemea uvuvi kufahamu mabadiliko ya hali ya hewa inavyo badili na mfumo wa uzazi wa maisha ya vinyama baharini na maji masafi na hivyo kuweza kua na athari katika mapato ya wafanya kazi hao.