Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikao cha 10 cha Baraza la Haki za Binadamu cha funguliwa Geneva

Kikao cha 10 cha Baraza la Haki za Binadamu cha funguliwa Geneva

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu Navi Pillay, ameyahimiza tena mataifa ya dunia kuweka kando tofuati zao na kufanya kazi pamoja kuhakikisha matokeo ya ufanisi katika mkutano wa mwezi ujao dhidi ya kutostahamiliana, ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni huko Geneva.

Akikifungua kikao cha kumi cha Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva siku ya Jumatatu, Kamishna Mkuu alisisitiza kwamba kushindwa kufikia maridhiano na kuhakikisha mafanikio kutakua na athari mbaya sana katika juhudi zote za haki za binadam na utaratibu wake kwa miaka kadha inayokuja. Bi Pillay ambae ni katibu mkuu wa mkutano ujao amesema inabidi kuacha nyuma mivutano na ugomvi ulopita ili kuweza kukabiliana na hali ya kutostahamiliana jambo ambalo anasema ni muhimu na linahitaji suluhisho la dharura. Tume maalum ya mataifa wanachama wa UM imeanza majadiliano huko Geneva kutayarisha rasimu ya hati ya mwisho ya mkutano wa mwezi ujao.