Hapa na pale

Hapa na pale

Kikosi cha pamoja cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika na UM huko Darfur kiliripoti Alhamisi kwamba utulivu wa kiasi fulani umerudi katika eneo lililokua na ghasia la Magharibi ya Sudan, ingawa kungali na wasi wasi juu ya kuendelea ghasia katika baadhi za sehemu. UNAMID inasema kumekua na ripoti za uhalifu huko Darfur ya Kaskazini na wanamgambo wenye silaha wanaendelea kuwashambulia na kuwabughudhi raia huko Darfur ya Kusini

Mjumbe maalum wa KM huko Iraq Staffan de Mistura, ameliambia Baraza la Usalama kwamba uchaguzi wa kipekee na wa amani ni hatua muhimu sana katika utaratibu wa kuleta ustawi nchini Irak. Hata hivyo mjumbe maalum ambae anaongoza ofisi ya UM huko Irak UNAMI, alionya kwamba utaratibu wa kisiasa haumaliziki kwa kufanyika uchaguzi. Kwani upigaji kura ni hatua moja kuelekea kujenga upatanishi wa kitaifa. Alikua anatoa ripoti yake juu ya maendeleo huko Irak.

Kasisi mmoja katika jeshi la zamani la Rwanda alihukumiwa kifungo cha miaka 25 jela kwa ajili ya utekaji nyara, mauwaji, ubakaji wa raia wa ki-Tutsi na mahakama ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya mauwaji ya kimbari ya Rwanda ya 1994. Taarifa ya ICTR inaeleza kamba, Emmanuel Rukundo alipatikana na hatia ya muawaji ya kimbari, mauwaji yanayochukuliwa kua ni uhalifu dhidi ya ubinadamu.

apa na pale