Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasi wasi wa ghasia mpya mashariki mwa JKK

Wasi wasi wa ghasia mpya mashariki mwa JKK

Idara ya huduma za dharura ya UM, OCHA imeeleza wasi wasi wakutokea ghasia mpya dhidi ya wafanyakazi wa huduma za dharura huko jimbo la Kivu ya Kaskazini nchini JKK.

Katika kipindi cha siku kumi mwezi huu kumekuwepo na mashambulizi saba dhidi ya wafanyakazi wa huduma zilizoripotiwa kukiwepo na mashambulizi 15 kama hayo tangu mwanzoni mwa mwaka. OCHA na wafanaykazi wa huduma za dharura wametoa mwito kwa pande zinazo gombana kusitisha mara moja mashambulio na kuruhusu wafanaykazi kutoa huduma za dharura na kuwalinda watu walokimbia makazi yao.