Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM amemtuma mshauri wake wa kisiasa kusaidia mzozo wa Madagascar

KM amemtuma mshauri wake wa kisiasa kusaidia mzozo wa Madagascar

KM Ban Ki-moon amemtuma mshauri wake wa cheo cha juu wa masuala ya kisiasa hadi Madagascar kufuatia ombi la serekali ya Antananarivo kuutaka UM kuchukua jukumu kubwa zaidi kusaidia kukabiliana na mvutano wa kisiasa katika kisiwa hicho cha Bahari ya Hindi.

Naibu katibu mkuu Haile Menkerios aliyekua anafuatana na KM katika ziara yake ya Afrika amepelekwa kutathmini hali ilivyo. Bw Ban alikutana na mawaziri wawili wa serekali ya Madagascar kwenye uwanja wa ndege wa Johannesburg jana, kabla ya kuondoka, na kueleza kwamba ameshamteua mjumbe maalum ataepelekwa karibuni. Rais Marc Ravalomanana na meya wa mji mkuu Antananarivo Andry Rajoelina walitangaza mapema mwezi huu kwamba wangelipendelea upatanishi wa UM kutanzua mzozo wao kwa njia ya amani.