Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

"Kijiji Muafaka" - mradi mpya wa walinda amani huko Liberia

"Kijiji Muafaka" - mradi mpya wa walinda amani huko Liberia

Katika juhudi za kumarisha uzalishaji na usalama wa chakula walinda amani wa UM kutoka Bangladesh huko Liberia wametenga eka 150 za ardhi kujenga kijiji kipya, kikiwa na shamba la ushirika, ufugaji wa kuku, na kidimbwi cha samaki.

Akifungua kijiji muafaka cha bangle Bong, Kamanda wa kikosi cha UNMIL Luteni Jenerali Abu Tayebzahirul Alam, aliwahimiza wakazi wa mji wa Maimu katika jimbo la Bong kuchukua kwa udhibiti wa mradi huo na kuutunza kwa dhati kwa ajili ya maendeleo yao ya baadae, ikiwa ni moja wapo ya hatua muhimu ya kuleta amani ya kudumu katika taifa hilo la Afrika Magharibi.