Mjumbe Maalum wa UM huko Sahara Magharibi anakamilisha mazungumzo Algeria

26 Februari 2009

Mjumbe maalum wa KM kwa ajili ya Sahara Magharibi, Christopher Ross, amesema mazungumzo yake na wakuu wa Algeria yalikua ya kina, wazi na ya manufaa.

Kabla ya kuondoka Algiers kuelekea Hispania kwa mazungumzo zaidi, Bw. Ross alisema majadiliano yalihusu msimamo wa Algeria kuelekea suala la Sahara Magharibi na njia bora kabisa ya kuanzisha tena utaratibu wa majadiliano. Mjumbe huyo alikumbusha kwamba majadiliano kati ya Morocco na chama cha Polisario yaliitishwa na Baraza la Usalama ili kutafuta suluhisho la kudumu la kisiasa litakalowapatia wananchi wa Sahrawi haki ya kujitawala.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter