Skip to main content

KM amewasili Tanzania kituo cha pili cha ziare ya Afrika

KM amewasili Tanzania kituo cha pili cha ziare ya Afrika

KM wa UM Ban Ki-moon, amewasili Tanzania kituO cha pili cha ziara yake ya Afrika akitokea Afrika Kusini.

Akiwa Tanzania kwa siku tatu atakutana na Rais Jakaya Kikwete na kukutana na mabalozi wa nchi za kigeni, maafisa wa serekali na wasomi. Bw. Ban anatazamiwa kutembelea Zanzibar pamoja na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Vita kwa ajili ya Rwanda (ICTR) huko Arusha. Kabla ya kuondoka Afrika Kusini akizungumza na waandishi habari mjini Pretoria KM alisema ziara yake ni ya kuhamasisha amani na ustawi katika mataifa yenye ghasia barani Afrika.