Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Baraza la usalama limelaani vikali shambulio la kujitoa mhanga dhidi ya kambi ya kikosi cha walinda amani wa Umoja wa afrika AU huko Mogadishu.

Wajumbe wa baraza walirudia tena kulaani mashambulizi ya kila aina dhidi ya AMISOM. Taarifa ya wajumbe 15 wa baraza hilo ilipongeza pia utaratibu wa kisiasa unaoendelea ulopelekea kupanuliwa bunge na kuchaguliwa rais mpya.

KM Ban KI-moon alitoa mwito kwa serekali ya Zimbabwe kuwaachilia huru wanaharakati wa upinzani na watetezi wa haki za binadam, akiahidi msaada wa UM wakati taifa hilo linajaribu kutanzua matatizo yake makubwa. KM alikua anazungumza baada ya kukutana na viongozi wa Afrika Kusini katika ziara yake rasmi ya mataifa matano ya afrika.

Rais wa baraza kuu la UM ametoa mwito kwa China kuunga mkono juhudi za UM kufanya mageuzi ya taasisi za fedha, uchumi na biashara ili kukabiliana na mzozo wa hivi sasa wa kiuchumi na kifedha duniani. Balozi Miguel D'Escoto alikua akihutubia mkutano katika chuo kikuu cha masuala ya kigeni ya China huko Bejing, akiwa katika kutayarisha mkutano wa June kujadili juu ya mageuzi ya mfumo wa fedha.

Afisi ya UM huko Cote D'ivore UNOCI imeanda mafunzo mepya ya kuimarisha kiwango cha wanawake katika kikosi cha polisi nchini humo. Kiasi ya maafisa 30 wa Cote D'Ivore wanashiriki katika mafunzo hayo ya jinsi wanayopokelewa pamoja na mazingira ya kazi ya wanawake katika kikosi cha taifa cha polisi, kazi iliyokua ya wanaume pekee..