Mtaalamu wa UM asema mauwaji na polisi Kenya hupandwa kwa kawaida

25 Februari 2009

Mtaalamu huru wa masuala ya mauwaji ya kiholela UM Philip Alston anasema mauwaji ya kiholela yanayofanywa na polisi wa Kenya ni mambo ya kawaida, yaliyoenea na hupangwa kwa makini.

Anasema yanafanyika kwa hiyari na bila ya kujali au kuhukumiwa mtu. Aligundua kwamba makundi maalum ya mauwaji ya polisi yaliundwa kutokana na amri za maafisa wa vyeo vya juu ili kuangamiza kundi la Mungiki. Alitoa mwito kwa rais wa Kenya kukiri kuenea kwa tatizo la mauwaji ya kiholela nchini humo na kuchukua hatua za dhati kufanya mabadiliko. Alisema uwongozi thabiti juu ya suala hilo unaweza tu kuchukuliwa kutoka kinara na mageuzi makubwa katika kikosi cha polisi ni lazima kuanza mara moja kwa kufukuzwa kamishna wa polisi. Na zaidi ya hayo mtaalamu maalum aligundua ushahidi wa kuaminika kwamba huko Mt Elgon, polisi na jeshi walitenda mateso na mauwaji ya kiholela yaliyopangwa dhidi ya raia wakati wa operesheni yao ya 2008 ya kuwafyeka wanamgambo wa Sabaot Land Defence Force.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter