Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe maalum wa UM ahimiza kusitishwa mapigano kusini mwa Sudan

Mjumbe maalum wa UM ahimiza kusitishwa mapigano kusini mwa Sudan

Mjumbe maalum wa KM wa Um huko Sudan ametoa mwito kwa pande zote kusitisha mara moja mapigano yaliyozuka jana katika mji wa kusini wa Malakal.

Katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya UM huko Sudan UNMIS, Ashraf Jehangir Qazi ametoa mwito pia kwa wote wanaohusika kuchukua hatua za kutanzua tofauti zao kwa njia ya kuwajibika. Bw Qazi alisema ni muhimu sana kwa uwongozi wa kijeshi wa Jeshi la Sudan na Jeshi la ukombozi la watu wa Sudan SPLA, kuhakikisha kwamba vikosi vya pamoja vilivyounganishwa vinatekeleza wajibu wao wa kufanya kazi pamoja kuwalinda raia. Katika taarifa yake ya karibuni juu ya Sudan Bw Ban alionya kwamba miaka mine baada ya kutia sahihi mkataba wa amani CAP, hali jumla ya usalama ingali dhaifu, na haina uhakika wakati kura ya maoni ya 2011 inakaribia ikiwa Kusini ya Sudan ijitenge au ibaki ndani ya umoja wa taifa.